Wanyangʼanyi wa Gadiantoni Ona pia Makundi maovu ya siri Katika Kitabu cha Mormoni, ni kundi la wanyangʼanyi lililoundwa na Mnefi mwovu aliyeitwa Gadiantoni. Shirikisho lao lilijengwa juu ya usiri na viapo vya kishetani. Gadiantoni alisababisha kuangamizwa kwa taifa la Wanefi, Hel. 2:12–13. Ibilisi alitoa viapo na maagano ya siri kwa Gadiantoni, Hel. 6:16–32. Ushirikiano wa siri ulisababisha kuangamia kwa taifa la Wayaredi, Eth. 8:15–26.