Msaada wa Masomo
Nefi, Mwana wa Lehi
iliyopita inayofuata

Nefi, Mwana wa Lehi

Katika Kitabu cha Mormoni, ni mwana mwaminifu wa Lehi na Saria (1 Ne. 1:1–4; 2:5). Nefi alikuwa na imani thabiti katika neno la Mungu (1 Ne. 3:7) na akawa nabii mkubwa, mtunza kumbukumbu, na kiongozi wa watu wake.

Kitabu cha 1 Nefi

Mlango wa 1 hadi 18:8 inajishughulisha zaidi na kuondoka kwa nabii Lehi na familia yake kutoka Yerusalemu. Walisafiri kupitia kwenye jangwa kame hadi walipofika baharini. 1 Nefi 18:9–23 inaelezea juu ya safari yao kwenda nchi ya ahadi, kama walivyoelekezwa na Bwana, licha ya uasi wa Lamani na Lemueli. Mlango wa 19–22 inaelezea madhumuni ya Lehi ya kutunza kumbukumbu (1 Ne. 6; 19:18)—ili kuwashawishi watu wote kumkumbuka Bwana Mkombozi wao. Alimnukuu Isaya (1 Ne. 20–21) na akatafsiri ujumbe wa Isaya, kwa matumaini kwamba watu wote wapate kuja kumjua Yesu Kristo kama Mwokozi na Mkombozi wao (1 Ne. 22:12).

Kitabu cha 2 Nefi

Mlango wa 1–4 ina baadhi ya mafundisho na unabii wake wa mwisho kabla ya kifo chake, ikiwa ni pamoja na baraka juu ya wanawe na wazao wao. Mlango wa 5 unafafanua kwa nini Wanefi walijitenga wenyewe kutoka kwa Walamani. Wanefi walijenga hekalu, walifundisha torati ya Musa, na walitunza kumbukumbu. Mlango wa 6–10 ina maneno ya Yakobo, mdogo wa Nefi. Yakobo alirejea upya historia ya Yuda na alitoa unabii juu ya Masiya, baadhi yake yamechukuliwa kutoka katika maandiko ya nabii Isaya. Katika mlango wa 11–33. Nefi ameandika ushuhuda wake juu ya Kristo, ushuhuda wa Yakobo, unatoa unabii juu ya siku za mwisho, na milango kadhaa kutoka katika Agano la Kale Kitabu cha Isaya.

Mabamba ya Nefi