Misaada ya Kujifunza
Amina


Amina

Humaanisha “na iwe hivyo” au “hivyo ndivyo.” Amina husemwa ili kuonyesha makubaliano na maafikiano ya moyo au ya dhati (Kum. 27:14–26) au ukweli (1 Fal. 1:36). Siku hizi mwishoni mwa sala, shuhuda, na mahubiri wale wote waliosikia sala au ujumbe husema amina ya kusikika ili kuonyesha makubaliano na maafikiano.

Katika nyakati za Agano la Kale, mtu alipaswa kusema amina wakati anapotoa kiapo (1 Nya. 16:7, 35–36; Neh. 5:12–13; 8:2–6). Kristo anaitwa “aliye Amina, aliye mwaminifu na shahidi wa kweli” (Ufu. 3:14). Amina pia ilitumika kama ishara ya agano katika Shule ya Manabii (M&M 88:133–135).