Misaada ya Kujifunza
Upangaji watoto


Upangaji watoto

Maandiko huzungumza juu ya aina mbili za upangaji watoto.

(1) Mtu ambaye si wa ukoo wa Ki-Israeli huweza kuwa mshirika wa familia ya Ibrahimu na wa nyumba ya Israeli kwa kuwa na imani katika Yesu Kristo, kutubu, kwa kubatizwa kwa kuzamishwa, na kumpokea Roho Mtakatifu (2 Ne. 31:17–18; M&M 84:73–74; Ibr. 2:6, 10–11).

(2) Wale wote waliopokea ibada za injili za wokovu huwa wana na mabinti za Yesu Kristo kwa kuendelea kutii amri Zake (Rum. 8:15–17; Gal. 3:24–29; 4:5–7; Mos. 5:7–8).