Misaada ya Kujifunza
Urejesho wa Injili


Urejesho wa Injili

Ni kurejeshwa upya na Mungu kwa kweli na ibada za injili Yake miongoni mwa wanadamu duniani. Injili ya Yesu Kristo ilipotea duniani kwa njia ya ukengeufu uliotokea baada ya huduma ya Mitume wa Kristo duniani. Ukengeufu huo ulifanya uwepo umuhimu wa urejesho wa injili. Kwa njia ya maono, huduma za malaika, na mafunuo kwa wanadamu duniani, Mungu alirejesha injili. Urejesho ulianza na Joseph Smith Nabii (JS—H 1; M&M 128:20–21) na umeendelea hadi sasa kwa njia ya kazi za manabii wa Bwana wanaoishi.