Misaada ya Kujifunza
Kusulubiwa


Kusulubiwa

Mtindo wa uuaji wa Kirumi uliokuwa maarufu katika nyakati za Agano Jipya, ambamo mtu alikuwa akiuawa kwa kufungwa au kupigiliwa misumari katika mikono yake na miguu yake kwenye msalaba. Kwa kawaida ilikuwa ikifanyika kwa watumwa tu na wahalifu wa daraja la chini kabisa. Kusulubiwa daima kulitanguliwa na kupigwa kwa mijeledi (Mk. 15:15). Mtu aliyekuwa akisulubiwa kwa kawaida alikuwa akibebeshwa msalaba wake kwenda mahali pa kuulia (Yn. 19:16–17). Mavazi yake kwa kawaida yalichukuliwa na askari waliokuwa wakitekeleza hukumu yake (Mt. 27:35). Msalaba ulisimamishwa kwa kufukiwa chini ardhini ili miguu ya mtu huyo iwe futi moja au mbili tu kutoka ardhini. Msalaba ulilindwa na askari hadi mtu wa juu ya msalaba amekufa, kitu ambacho mara nyingine kilichukua hadi siku tatu (Yn. 19:31–37).

Yesu Kristo alisulibiwa kwa sababu kikundi cha wasioamini kimakosa kabisa walimshtaki kwa uasi dhidi ya Kaisari na kukufuru kwa sababu Yeye alisema kuwa Yeye alikuwa Mwana wa Mungu. Joho la zambarau (Yn. 19:2), taji la miiba, na matukano mengine yalitolewa kwa Yesu (Mt. 26:67; Mk. 14:65).