Misaada ya Kujifunza
Nehemia


Nehemia

Muisraeli aliyekuwa mtu maarufu katika Babiloni katika Agano la Kale (alikuwa Mlawi au wa kabila la Yuda) aliyekuwa na ofisi ya mnyweshaji wa mfalme katika baraza la Artashasta, ambaye kutoka kwake alipata mamlaka ya kifalme yaliyomruhusu yeye kujenga upya kuta za Yerusalemu.

Kitabu cha Nehemia

Kitabu hiki ni mwendelezo wa kitabu cha Ezra. Kina maelezo juu ya maendeleo na ugumu wa kazi huko Yerusalemu kikifuatiwa na kurudi kwa Wayahudi kutoka utumwa wa Babilonia. Mlango wa 1–7 inasimulia juu ya safari ya kwanza ya Nehemia huko Yerusalemu na kujengwa upya kwa kuta za jiji licha ya upinzani mkubwa. Mlango wa 8–10 inaelezea marekebisho ya kidini na kijamii ambayo Nehemia alijaribu kuyatekeleza. Mlango wa 11–13 inatoa orodha ya majina ya wale wanaostahili na kutoa taarifa ya kuwekwa wakfu kwa ukuta. Mistari ya 4–31 ya mlango wa 13 inaandikwa juu ya safari ya pili ya Nehemia kwenda Yerusalemu baada ya kuwa mbali kwa miaka kumi na miwili.