Misaada ya Kujifunza
Hesabu kwa haki, Kuhesabiwa haki


Hesabu kwa haki, Kuhesabiwa haki

Kusamehewa adhabu kwa ajili ya dhambi na kutamkwa kuwa huna hatia. Mtu anahesabiwa haki kwa neema ya Mwokozi kwa njia ya imani katika Yeye. Imani hii huonyeshwa katika toba na utiifu kwa sheria na ibada ya injili. Upatanisho wa Yesu Kristo huwawezesha wanadamu kutubu na kuhesabiwa haki au kusamehewa kutokana na adhabu ambayo vinginevyo wangeipata.