Uteuzi ufanywao na Mungu kwa watoto wake wa kiroho waliokuwa mahodari kabla ya kuzaliwa katika mwili ili kutimiza kazi fulani wakati wa maisha yao katika mwili wenye kufa.
Mungu aliweka mipaka ya watu, Kum. 32:8 .
Kabla sijakuumba katika tumbo, nilikuteua kabla wewe kuwa nabii, Yer. 1:5 .
Mungu aliziamuru nyakati kabla ya kuwekwa, Mdo. 17:26 .
Maana wale aliowajua tangu asili, yeye pia aliwachagua tangu asili, Rum. 8:28–30 .
Yeye alituchagua sisi katika yeye kabla ya kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, Efe. 1:3–4 .
Yesu Kristo aliteuliwa kabla kuwa Mkombozi, 1 Pet. 1:19–20 (Ufu. 13:8 ).
Mwanangu Mpendwa alichaguliwa tangu mwanzo, Musa 4:2 .
Ibrahimu alichaguliwa kabla hajazaliwa, Ibr. 3:23 .