Misaada ya Kujifunza
Lulu ya Thamani Kuu


Lulu ya Thamani Kuu

Ufalme wa Mungu duniani unalinganishwa na “lulu ya thamani kuu” (Mt. 13:45–46).

Lulu ya Thamani Kuu pia ni jina lililotolewa kwa moja ya vitabu vinne vya maandiko yanayoitwa “vitabu vitakatifu” vya Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Toleo la kwanza la Lulu ya Thamani Kuu lilichapishwa katika mwaka 1851 na lilikuwa na baadhi ya mambo ambayo sasa yapo katika Mafundisho na Maagano. Matoleo yaliyochapishwa tangu mwaka 1902 yana (1) dondoo kutoka tafsiri ya Joseph Smith ya Kitabu cha Mwanzo, kinachoitwa Kitabu cha Musa, na cha Mathayo 24, kinachoitwa Joseph Smith—Mathayo; (2) tafsiri ya Joseph Smith ya papiri fulani ya Kimisri ambayo aliiipata katika mwaka 1835, kinachoitwa Kitabu cha Ibrahimu; (3) dondoo kutoka katika historia ya Joseph Smith juu ya Kanisa ambayo aliiandika katika mwaka wa 1838, inayoitwa Joseph Smith—Historia ya; na (4) Makala ya Imani, matamko kumi na matatu juu ya imani na mafundisho.