Misaada ya Kujifunza
Ahabu


Ahabu

Mmoja kati ya wafalme waovu na aliyekuwa na nguvu nyingi katika Israeli ya kaskazini, katika Agano la Kale. Alimwoa Yezebeli, binti mfalme wa Sidoni, ambaye kwa ushawishi wake kuabudiwa kwa Baali na Ashtorethi kulianza katika Israeli (1 Fal. 16:29–33; 2 Fal. 3:2) na alijaribu kuwaangamiza manabii na kuabudiwa kwa Yehova (1 Fal. 18:13).