Misaada ya Kujifunza
Msimamizi, Usimamizi


Msimamizi, Usimamizi

Mtu anayeangalia mambo au mali ya mtu mwingine. Kile ambacho msimamizi anakiangalia ndicho huitwa usimamizi. Vitu vyote duniani ni mali ya Bwana; sisi tu wasimamizi Wake. Sisi tunawajibika kwa Bwana, lakini tunaweza kutoa taarifa juu ya usimamizi wetu kwa wawakilishi wa Mungu walio na mamlaka. Tunapopata wito wa utumishi kutoka kwa Bwana au watumishi Wake wenye mamlaka, usimamizi huo waweza kujumuisha mambo yote kiroho na kimwili (M&M 29:34).