Rudi, Kurudiwa Ona pia Shida Rekebisho au fundisho la nidhamu litolewalo kwa watu binafsi au vikundi ili kuwasaidia waweze kujirekebisha au kuwa imara zaidi. Msidharau kurudiwa na mkono wa Mwenyezi, Ayu. 5:17 (Mit. 3:11). Heri mtu yule umwadhibuye, Ee Bwana, Zab. 94:12. Maandiko yote yametolewa kwa ajili ya kuwaonya, na kuwaadabisha, 2 Tim. 3:16. Bwana huwarudi wale awapendao, Ebr. 12:5–11. Bwana anaonelea kuwa ni vyema kuwarudi watu wake, Mos. 23:21–22. Bwana asipowarudi watu wake, wao hawatamkumbuka yeye, Hel. 12:3. Bwana alisema na kaka wa Yaredi, na akamrudi, Eth. 2:14. Aliwarudi ili wapate kutubu, M&M 1:27. Wale niwapendao pia huwarudi ili dhambi zao zipate kusamehewa, M&M 95:1. Wale wote wasiostahmili kurudiwa hawawezi kutakaswa, M&M 101:2–5. Watu wangu yafaa kuwarudi hadi wajifunze utiifu, M&M 105:6. Yule ambaye hatavumilia kuadhibiwa haustahili ufalme wangu, M&M 136:31.