Misaada ya Kujifunza
Yakobo, Mwana wa Zebedayo


Yakobo, Mwana wa Zebedayo

Mmoja wa Mitume Kumi na Wawili waliochaguliwa na Yesu wakati wa huduma Yake katika mwili ufao. Alikuwa kaka yake Yohana. Alikuwa mmoja wa Mitume watatu waliochaguliwa kuwa na Yesu katika matukio fulani maalumu: wakati wa kufufuliwa kwa binti wa Yairo (Mk. 5:37), wakati wa Kugeuka Sura (Mt. 17:1; Mk. 9:2; Lk. 9:28), na wakati wa Gethsemani (Mt. 26:37; Mk. 14:33). Pamoja na Petro na Yohana, alirejesha ukuhani wa Melkizedeki duniani kwa kumtawaza Joseph Smith na Oliver Cowdery (M&M 27:12; 128:20; JS—H 1:72).