Msaada wa Masomo
Walamani
iliyopita inayofuata

Walamani

Kikundi cha watu katika Kitabu cha Mormoni, wengi wao wakiwa ni wazao wa Lamani, mwana mkubwa wa Lehi. Walijiona kuwa walikuwa wametendewa makosa na Nefi na wazao wake (Mos. 10:11–17). Kama matokeo yake, wakawaasi Wanefi na mara kwa mara walikataa mafundisho ya injili. Hata hivyo, muda mfupi kabla ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, Walamani waliikubali injili nao wakawa watu wema zaidi kuliko Wanefi (Hel. 6:34–36). Miaka mia mbili baada ya Kristo kuitembelea Marekani, wote Walamani na Wanefi wakawa waovu na wakaanza kupigana vita baina yao. Karibia mwaka 400 B.K., Walamani waliliangamiza kabisa taifa la Wanefi.