Misaada ya Kujifunza
Isaka


Isaka

Patriaki wa Agano la Kale. Kuzaliwa kwake kwa Ibrahimu na Sara wakiwa katika umri wa uzee ulikuwa ni muujiza (Mwa. 15:4–6; 17:15–21; 21:1–8). Kukubali kwa Ibrahimu kumtoa sadaka Isaka kulikuwa ni mfano wa Mungu na Mwanawe wa Pekee (Yak. [KM] 4:5). Isaka alikuwa mrithi wa ahadi za agano la Ibrahimu (Mwa. 21:9–12; 1 Ne. 17:40; M&M 27:10).