Misaada ya Kujifunza
Kuhudumu


Kuhudumu

Kufanya kazi ya Bwana duniani. Watumishi wateule wa Bwana ni lazima waitwe na Mungu ili kuhudumu katika kazi Yake. Wahudumu wa kweli wafanyapo mapenzi ya Bwana, humwakilisha Bwana katika kazi zao rasmi na humwakilisha kama mawakala Wake (M&M 64:29), hivyo basi huendesha kazi muhimu kwa wokovu wa wanadamu. Bwana ametoa mitume, manabii, wainjilisti, makuhani wakuu, sabini, wazee, maaskofu, makuhani, walimu, mashemasi, wasaidizi na utawala kwa ajili ya kuwakamilisha Watakatifu, kwa ajili ya kazi ya huduma (1 Kor. 12:12–28; Efe. 4:11–16; M&M 20; 107).