Sayari ambayo juu yake tunaishi, iliumbwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo ili itumiwe na mwanadamu wakati wa kuzaliwa katika mwili wenye kufa na kwa majaribio yake. Hatima yake ni kuwa iliyotukuzwa na kuinuliwa. (M&M 77:1–2 ; 130:8–9 ). Dunia itakuwa ni urithi wa milele wa wale walioishi wakistahili fahari ya selestia (M&M 88:14–26 ). Watafurahia uwepo wa Baba na Mwana (M&M 76:62 ).
Iliumbwa kwa ajili ya mwanadamu
Mungu alimpa mwanadamu utawala juu ya dunia, Mwa. 1:28 (Musa 2:28 ).
Dunia ni ya Bwana, Ku. 9:29 (Zab. 24:1 ).
Bwana amewapa dunia wanadamu, Zab. 115:16 .
Mimi nimeiumba dunia na nimemtunuku mwanadamu juu yake, Isa. 45:12 .
Dunia itatolewa kwa wale waliomchukua Roho Mtakatifu kuwa kiongozi wao, M&M 45:56–58 (M&M 103:7 ).
Wale ambao wameitii injili wanapokea ujira wa mambo mema ya dunia, M&M 59:3 .
Walio maskini na wapole wa dunia watairithi, M&M 88:17 (Mt. 5:5 ; 3Â Ne. 12:5 ).
Bahari ya kioo ni dunia katika hali yake ya kutakaswa, isiyokufa, na ya milele, M&M 77:1 .
Dunia lazima itakaswe na kuandaliwa kwa ajili ya utukufu wa selestia, M&M 88:18–19 .
Maji na yakusanyike mahali pamoja, Mwa. 1:9 .
Katika siku za Pelegi dunia iligawanyika, Mwa. 10:25 .
Dunia itakunjwa pamoja kama karatasi na kupita, 3Â Ne. 26:3 (M&M 29:23 ).
Patakuwepo na mbingu mpya na dunia mpya, Eth. 13:9 (M&M 29:23 ).
Bahari ya kioo ni dunia katika hali yake ya kutukaswa, kutokufa, na ya milele, M&M 77:1 .
Dunia lazima itakaswe na kuandaliwa kwa ajili ya fahari ya utukufu wa selestia, M&M 88:18–19 .
Dunia hii itafanywa kuwa mfano wa jiwe angavu nayo itakuwa Urimu na Thumimu, M&M 130:8–9 .