Misaada ya Kujifunza
Wathesalonike, Waraka kwa


Wathesalonike, Waraka kwa

Vitabu viwili katika Agano Jipya. Mwanzoni zilikuwa ni barua ambazo Paulo aliziandika kwa Wathesalonike wakati akiwa katika Korintho wakati wa safari yake ya kwanza katika Ulaya takribani mwaka wa 50 B.K. Kazi yake katika Thesalonike inaelezwa katika Matendo 17. Paulo alitaka kurudi Thesalonike lakini alishindwa kufanya hivyo (1 The. 2:18). Kwa hiyo yeye akamtuma Timoteo kuwasalimia waongofu hao na kumletea taarifa ya jinsi walivyokuwa wakiendelea. Paulo aliandika waraka wa kwanza kama matokeo ya shukrani zake juu ya kurudi kwa Timoteo.

Wathesalonike wa Kwanza

Mlango wa 1–2 ina salamu za Paulo na sala yake kwa ajili ya Watakatifu hao; mlango wa 3–5 inafundisha juu ya makuzi ya kiroho, upendo, usafi wa kimwili, juhudi, na Ujio wa Pili wa Yesu Kristo.

Wathesalonike wa Pili

Mlango wa 1 una sala kwa ajili ya Watakatifu. Mlango wa 2 unazungumzia juu ya kuja kwa ukengeufu. Mlango wa 3 una sala ya Paulo kwa ajili ya ushindi wa malengo ya injili.