Misaada ya Kujifunza
Yeremia


Yeremia

Nabii wa Agano la Kale aliyezaliwa katika familia ya kikuhani na alitoa unabii wake katika Yuda tangu mwaka 626–586 K.K. Aliishi karibu na wakati wa manabii wengine wakuu: Lehi, Ezekieli, Hosea, na Danieli.

Yeremia alitawazwa kuwa nabii kabla ya kuzaliwa (Yer. 1:4–5). Wakati wa miaka yake ipatayo arobaini kama nabii alifundisha dhidi ya ibada za sanamu na utovu wa maadili miongoni mwa watu wa Uyahudi (Yer. 3:1–5; 7:8–10). Mara zote alikabiliana na upinzani na matukano (Yer. 20:2; 36:18–19; 38:4). Baada ya anguko la Yerusalemu, Wayahudi waliokimbilia Misri walimchukua Yeremia pamoja nao (Yer. 43:5–6), ambako, kulingana na mapokeo, walimpiga kwa mawe hadi kufa.

Kitabu cha Yeremia

Mlango wa 1–6 kuna unabii uliotolewa wakati wa utawala wa Yosia. Mlango wa 7–20 ni unabii wa wakati wa Yehoyakimu. Mlango wa 21–38 ni kuhusu utawala wa Zedekia. Mlango wa 39–44 kuna unabii na inaelezea matukio ya kihistoria baada ya anguko la Yerusalemu. Mlango wa 45 ina ahadi aliyompa Baruku, mwandishi wake, kwamba uhai wa Baruku ungelindwa. Mwishowe, mlango wa 46–51 ni unabii dhidi ya mataifa ya kigeni. Mlango wa 52 ni hitimisho la kihistoria. Sehemu ya unabii wa Yeremia ulikuwa katika mabamba ya shaba nyeupe ya Labani yaliyosalimishwa na Nefi (1 Ne. 5:10–13). Yeremia pia ametajwa mara mbili nyingine katika Kitabu cha Mormoni (1 Ne. 7:14; Hel. 8:20).

Kitabu cha Yeremia pia kinajumuisha uthibitisho wa kuishi kwa mtu kabla ya kuzaliwa na kuteuliwa kabla kwa Yeremia (Yer. 1:4–5); unabii wa kurudi kwa Waisraelii kutoka katika hali ya kutawanyika, kukusanywa kwa mmoja kutoka katika mji na wawili katika familia hadi Sayuni, nchi ya kupendeza ambayo Israeli na Yuda wangeliweza kukaa katika usalama na amani (Yer. 3:12–19); ni unabii wa Bwana wa kuwakusanya Israeli kutoka nchi za kaskazini kwa kuwapeleka “wavuvi” na “wawindaji” wengi kuwatafuta (Yer. 16:14–21). Tukio hili la siku za mwisho litakuwa pana sana kwa uwiano kuliko hata lile la Musa kuwaleta Israeli kutoka katika Misri (Yer. 16:13–15; 23:8).