Misaada ya Kujifunza
Yoshua


Yoshua

Nabii na kiongozi katika Agano la Kale, na mrithi wa Musa. Alizaliwa Misri kabla kutoroka kwa wana wa Israeli (Hes. 14:26–31). Yeye na Kalebu walikuwa miongoni mwa wapelelezi kumi na wawili waliotumwa Kanani. Wao tu ndiyo waliotoa taarifa nzuri juu ya ile nchi (Hes. 13:8, 16–33; 14:1–10). Alikufa katika umri wa miaka 110 (Yos. 24:29). Yoshua alikuwa mfano mkubwa wa nabii mpiganaji hodari.

Kitabu cha Yoshua

Kitabu hiki kimepewa jina la Yoshua kwa sababu yeye ndiye mtu muhimu ndani yake na siyo kwa sababu yeye alikuwa mtunzi. Mlango wa 1–12 inaelezea kukamatwa kwa Kaanani; mlango wa 13–24 inazungumzia makabila ya Israeli yakigawana nchi na ushauri wa mwisho wa Yoshua.

Mistari miwili maarufu katika kitabu cha Yoshua ni amri ya Bwana kwake ya kuyatafakari maandiko (Yos. 1:8) na wito wa Yoshua kwa watu wa kuwa waaminifu kwa Bwana (Yos. 24:15).