Kikundi cha watu katika Kitabu cha Mormoni, wengi wao wakiwa ni wazao wa nabii Nefi, mwana wa Lehi. Walijitenga na Walamani na kwa ujumla walikuwa waadilifu zaidi kuliko Walamani. Hata hivyo, mwishowe waliangamizwa na Walamani kwa sababu ya uovu.
Wanefi walijitenga na Walamani, 2 Ne. 5:5–17 .
Wale wote ambao hawakuwa Walamani walikuwa Wanefi, Yak. (KM) 1:13 .
Wanefi waliongozwa kwa kusudi lililo bora, Alma 43:6–9, 45 .
Wanefi kamwe hawakuwahi kuwa na furaha zaidi kuliko wakati wa Moroni, Alma 50:23 .
Wanefi waliokolewa kwa sababu ya sala za wenye haki, Alma 62:40 .
Wanefi wakaanza kufifia katika kutoamini, Hel. 6:34–35 .
Yesu alifundisha na kuhudumu miongoni mwa Wanefi, 3 Ne. 11:1–28:12 .
Wote waliongolewa kwa Bwana na walikuwa na mambo yote sawa, 4 Ne. 1:2–3 .
Hapakuwa na ugomvi, upendo wa Mungu ulikaa mioyoni mwao, nao walikuwa watu wenye furaha zaidi, 4 Ne. 1:15–16 .
Wanefi wakaanza kuwa wenye kiburi na kuwa bure, 4Â Ne. 1:43 .
Damu na mauaji ya watu wengi yalienea kote katika uso wote wa nchi, Morm. 2:8 .
Wanefi waliongezeka katika uovu na Mormoni alikataa kuwaongoza, Morm. 3:9–11 .
Wanefi wote, isipokuwa wale ishirini na wanne, waliuawa, Morm. 6:7–15 .
Kila Mnefi ambaye hangeweza kumkana Kristo aliuawa, Moro. 1:2 .
Wanefi waliangamizwa kwa sababu ya uovu na dhambi zao, M&M 3:18 .
Jihadhari na kiburi kwa kuogopa usije ukawa kama Wanefi, M&M 38:39 .