Misaada ya Kujifunza
Mauti ya Kimwili


Mauti ya Kimwili

Kutengana kwa mwili na roho. Anguko lilileta hali ya kufa na mauti duniani (2 Ne. 2:22; Musa 6:48). Upatanisho wa Yesu Kristo uliishinda mauti ili kwamba kila mmoja atafufuka (1 Kor. 15:21–23). Ufufuko ni zawadi ya bure kwa watu wote bila kujali kama wametenda mema au maovu katika maisha haya (Alma 11:42–44). Kila mtu huteseka mara moja tu kwa mauti ya kimwili kwa vile mara tufufukapo, miili yetu haiwezi kufa tena (Alma 11:45).