Misaada ya Kujifunza
Manase


Manase

Katika Agano la Kale, ni mwana mkubwa wa Asinati na Yusufu aliyeuzwa Misri (Mwa. 41:50–51). Yeye na kaka yake Efraimu walikuwa ni wajukuu wa Yakobo (Israeli) lakini walichukuliwa na kubarikiwa naye kama vile walikuwa wanawe mwenyewe (Mwa. 48:1–20).

Kabila la Manase

Wazao wa Manase walihesabiwa miongoni mwa makabila ya Israeli (Hes. 1:34–35; Yos. 13:29–31). Baraka za Musa kwa kabila la Yusufu, ambazo zilitolewa pia kwa Efraimu na Manase, zimeandikwa katika Kumbukumbu la Torati 33:13–17. Nchi waliyopangiwa ilikuwa sehemu kidogo upande wa magharibi ya Yordani na karibu na nchi ya Efraimu. Pia walikuwa na makoloni mashariki ya Yordani katika nchi yenye rutuba ya Bashani na Gileadi. Katika siku za mwisho, kabila la Manase litasaidia kabila la Efraimu katika kuwakusanya Israeli waliotawanyika (Kum. 33:13–17). Nabii Lehi wa Kitabu cha Mormoni alikuwa ni wa uzao wa Manase (Alma 10:3).