Misaada ya Kujifunza
Edeni


Edeni

Nyumbani kwa wazazi wetu wa kwanza, Adamu, na Hawa (Mwa. 2:8–3:24; 4:16; 2 Ne. 2:19–25; Musa 3–4; Ibr. 5), Edeni ilitengenezwa kama bustani, nayo ilikuwa katika upande wa mashariki. Adamu na Hawa walitolewa nje ya Edeni baada ya kula tunda lililokatazwa na wakawa na miili yenye kufa (Musa 4:29). Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha maelezo ya biblia juu ya Bustani ya Edeni. Unaongezea taarifa muhimu kwamba bustani hiyo ilikuwa mahali ambako sasa ni bara la Marekani ya Kaskazini.