Baba wa Mbinguni Ona pia Mungu, Uungu Baba wa roho za wanadamu wote (Zab. 82:6; Mt. 5:48; Yn. 10:34; Rum. 8:16–17; Gal. 4:7; 1 Yoh. 3:2). Yesu ndiye Mwanawe wa Pekee katika mwili. Mwanadamu ameamriwa kutii na kutoa heshima kwa Baba na kumwomba Yeye katika jina la Yesu. Kama mkiwasamehe watu, Baba yenu wa Mbinguni pia atawasamehe ninyi, Mt. 6:14 (Mt. 18:35; 3 Ne. 13:14). Baba yenu wa Mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji haya yote, Mt. 6:26–33 (3 Ne. 13:26–33). Je, Baba wa Mbinguni hatazidi sana kuwapa Roho Mtakatifu hao Wamwombao, Lk. 11:11–13. Atukuzwe Mungu, na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Efe. 1:3. Mnadaiwa milele na Baba yenu wa Mbinguni, Mos. 2:34. Kristo alilitukuza jina la Baba, Eth. 12:8. Watakatifu wanapaswa kutoa ushuhuda wa mateso yao kabla Baba hajaja kutoka katika mahali pa maficho yake, M&M 123:1–3, 6. Tulipata baraka kuu na tukufu kutoka kwa Baba yetu wa Mbinguni, JS—H 1:73.