Misaada ya Kujifunza
Mwana wa Mtu


Mwana wa Mtu

Jina ambalo Yesu Kristo alilitumia wakati alipokuwa akizungumza juu Yake mwenyewe (Lk. 9:22; 21:36). Lilimaanisha Mwana wa Mtu wa Utakatifu. Ni moja ya majina ya Mungu Baba. Wakati Yesu Alipojiita mwenyewe Mwana wa Mtu, lilikuwa ni tamko la wazi la uhusiano Wake mtakatifu na Baba. Jina hili linaonekana mara kwa mara katika vitabu vya Injili. Ufunuo wa siku za mwisho unathibitisha maana rasmi na utakatifu wa jina hili la Mwokozi (M&M 45:39; 49:6, 22; 58:65; Musa 6:57).