Kuwa na Roho wa Bwana husababisha mabadiliko makubwa katika moyo wa mtu kiasi kwamba akawa hana hamu tena ya kufanya uovu, bali akatamani kutafuta mambo ya Mungu.
Wale waliaminio jina la Kristo walizaliwa, siyo kwa damu, bali kwa Mungu, Yn. 1:12–13 .
Mtu asipozaliwa kwa maji na Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu, Yn. 3:3–7 .
Twaweza kuzaliwa tena kwa neno la Mungu, 1 Pet. 1:3–23 .
Yeyote aliyezaliwa kwa Mungu haendelei katika dhambi, TJS, 1Â Yoh. 3:9 .
Kwani yeyote aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu, 1Â Yoh. 5:4 .
Wale wazaliwao kwa Kristo hufanya agano na Mungu, Mos. 3:19 ; 5:2–7 .
Watu wote lazima wazaliwe tena; ndiyo, wazaliwe kwa Mungu, Mos. 27:25–26 (Alma 5:49 ).
Je, ninyi kiroho mmezaliwa kwa Mungu, Alma 5:12–19 .
Kama ninyi hamjazaliwa tena, hamwezi kuurithi ufalme wa mbinguni, Alma 7:14 .