Matukio au uzoefu ambao Mungu huwapa watu ili kuonyesha kwamba kitu fulani muhimu katika kazi Zake kimetokea au karibu kitatokea. Katika siku za mwisho, ishara nyingi kwa ajili ya Ujio wa Pili wa Mwokozi zimetolewa unabii. Ishara hizi huwaruhusu watu walio waaminifu kutambua mpango wa Mungu, kuonywa, na kujitayarisha.
Mlima wa nyumba ya Bwana utawekwa imara juu ya milima, Isa. 2:2–3 .
Bwana atatweka bendera na kuwakusanya Israeli, Isa. 5:26 (2 Ne. 15:26–30 ).
Jua litatiwa giza na mwezi utaacha nuru yake isiangaze, Isa. 13:10 (Yoe. 3:15 ; M&M 29:14 ).
Watu watavunja sheria na watalivunja agano lisilo na mwisho, Isa. 24:5 .
Wanefi watanena kama sauti kutoka mavumbini, Isa. 29:4 (2Â Ne. 27 ).
Israeli itakusanywa kwa nguvu, Isa. 49:22–23 (1 Ne. 21:22–23 ; 3 Ne. 20–21 ).
Mungu atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa, Dan. 2:44 (M&M 65:2 ).
Vita, ndoto, na maono vitautangulia Ujio wa Pili, Yoe. 2 .
Mataifa yote yatakusanyika kupigana na Yerusalemu, Zek. 14:2 (Eze. 38–39 ).
Siku ile inakuja ambayo itawaka kama tanuri, Mal. 4:1 (3 Ne. 25:1 ; M&M 133:64 ; JS—H 1:37 ).
Majanga makuu yatautangulia Ujio wa Pili, Mt. 24 (JS—M 1 ).
Paulo aliuelezea ukengeufu na nyakati za siku za mwisho zenye hatari, 2 Tim. 3–4 .
Manabii wawili watauawa na kufufuka katika Yerusalemu, Ufu. 11 (M&M 77:15 ).
Injili itarejeshwa katika siku za mwisho kwa huduma ya malaika, Ufu. 14:6–7 (M&M 13 ; 27 ; 110:11–16 ; 128:8–24 ).
Babilonia itaimarishwa na kuanguka, Ufu. 17–18 .
Israeli itakusanywa kwa nguvu, 1 Ne. 21:13–26 (Isa. 49:13–26 ; 3 Ne. 20–21 ).
Hii ni ishara, ili mpate kujua ule wakati, 3Â Ne. 21:1 .
Kitabu cha Mormoni kitatokea kwa uwezo wa Mungu, Morm. 8 .