Mtu kuwa mpole na mwenye kufundishika, au hali ya kuwa mpole na mwenye kufundishika. Unyenyekevu ni pamoja na kutambua utegemezi wetu kwa Mungu na kutamani kujiweka katika mapenzi Yake.
Mungu alikuongoza jangwani kwa miaka arobaini ili kukufanya uwe mnyenyekevu, Kum. 8:2 .
Niliinyenyekeza nafsi yangu kwa kufunga, Zab. 35:13 .
Heri kijana maskini mwenye hekima kuliko mfalme mzee mpumbavu, Mh. 4:13 .
Bwana hukaa pamoja na yule aliye mnyenyekevu, Isa. 57:15 .
Yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto mdogo huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni, Mt. 18:4 .
Yeyote atakayejinyenyekeza mwenyewe atakwezwa, Mt. 23:12 (Lk. 14:11 ; 18:14 ).
Yesu alijinyenyekeza mwenyewe na akawa mtii hadi mauti, Flp. 2:8 (Lk. 22:42 ; 23:46 ).
Mungu huwapinga wenye kiburi, na huwapa wanyenyekevu neema, 1 Pet. 5:5–6 (2 Ne. 9:42 ).
Jinyenyekezeni wenyewe katika vina vya unyenyekevu, Mos. 4:11 (2Â Ne. 9:42 ; 3Â Ne. 12:2 ).
Je, mmekuwa wanyenyekevu vya kutosha, Alma 5:27–28 .
Sehemu kubwa ya watu waliokuwa wanyenyekevu zaidi wakawa imara zaidi katika unyenyekevu wao, Hel. 3:33–35 .
Ninawapa wanadamu udhaifu ili wapate kuwa wanyenyekevu, Eth. 12:27 .
Unyenyekevu ni sifa kwa ajili ya ubatizo, M&M 20:37 .
Jinyenyekezeni mbele yangu na nanyi mtaniona na kujua ya kuwa Mimi ndimi, M&M 67:10 .
Uwe mnyenyekevu na Bwana atakupa jibu la sala zako, M&M 112:10 .
Mtu aliye mjinga na ajifunze hekima kwa kujinyenyekeza mwenyewe, M&M 136:32 .
Roho amepelekwa ili kuwaangaza walio wanyenyekevu, M&M 136:33 .