Misaada ya Kujifunza
Tamko Rasmi 2


Tamko Rasmi 2

Maelezo ya mafundisho ya kidini yanayohusu ni nani anaweza kushika ukuhani wa Mungu, maelezo ambayo sasa yamepigwa chapa katika kurasa za mwisho za Mafundisho na Maagano. Mapema Juni 1978, Bwana alimfunulia Rais Spencer W. Kimball kwamba ukuhani utolewe kwa wanaume wote walio waumini wa Kanisa wenye kustahili. Hii ilifanya ukuhani upatikane kwa waumini wanaume wote wenye kustahili na baraka za hekaluni zipatikane kwa waumini wote wenye kustahili, bila kujali asili au rangi. Mnamo 30 Septemba 1978, tamko hili liliwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa Kanisa na lilikubaliwa kwa kura zote.