Misaada ya Kujifunza
Tito, Waraka kwa


Tito, Waraka kwa

Wakati Paulo alipokuwa huru kwa muda kutoka kifungo cha gereza la Kirumi, aliandika waraka kwa Tito, aliyekuwa katika Krete. Barua inaadiri zaidi maswali yanayohusiana na nidhamu ya kibinafsi na muundo wa Kanisa.

Mlango wa 1 una salamu za Paulo na mafundisho ya jumla juu ya sifa za maaskofu. Mlango wa 2–3 ina mafundisho ya kawaida na ujumbe binafsi kwa Tito juu ya jinsi ya kuyatenda makundi mbalimbali ya Kanisa la Krete. Paulo aliwatia moyo Watakatifu ili waushinde ukaidi, wawe na kiasi na waaminifu, na waendeleze matendo mema.