Misaada ya Kujifunza
Abednego


Abednego

Katika Agano la Kale, Shadraki, Meshaki, na Abednego walikuwa vijana watatu wa Kiisraeli ambao, pamoja na Danieli, waliletwa katika jumba la Nebukadneza, mfalme wa Babilonia. Jina la Abednego katika Kiebrania lilikuwa Azaria. Vijana hawa wanne walikataa kujinajisi kwa kula chakula na mvinyo wa mfalme (Dan. 1). Mfalme aliwatupa Shadraka, Meshaki, na Abednego katika tanuru lenye kuwaka moto lakini kimiujiza wakaokolewa (Dan. 3).