Misaada ya Kujifunza
Lutu


Lutu

Katika Agano la Kale, ni mwana wa Harani na mpwawe Ibrahimu (Mwa. 11:27, 31; Ibr. 2:4). Harani alikufa kwa sababu ya baa la njaa katika Uru (Ibr. 2:1). Lutu aliondoka Uru pamoja na Ibrahimu na Sara na akasafiri pamoja nao hadi Kaanani (Mwa. 12:4–5). Lutu alichagua kuishi Sodoma. Bwana aliwatuma wajumbe kwenda kumwonya Lutu aikimbie Sodoma kabla Bwana hajaiteketeza kwa sababu ya uovu wa watu (Mwa. 13:8–13; 19:1, 13, 15), hata hivyo, mkewe Lutu aliangalia nyuma wakati wa angamizo na akawa nguzo ya chumvi (Mwa. 19:26). Agano Jipya linayo marejeo kwa Lutu (Lk. 17:29; 2 Pet. 2:6–7). Maisha yake baada ya kutengana na Ibrahimu yanaelezwa katika Mwanzo 13, 14 na 19.