Misaada ya Kujifunza
Pentekoste


Pentekoste

Kama sehemu ya torati ya Musa, Sikukuu ya Pentekoste au Mavuno ya Kwanza ilifanyika siku hamsini baada ya Sikukuu ya Pasaka (Law. 23:16). Pentekoste ilikuwa ni kusherehekea mavuno, na katika Agano la Kale inaitwa Sikukuu ya Mavuno au Sikukuu ya Majuma. Ilikuwa ni sikukuu hii ambayo ilikuwa ikisherehekewa wakati wale Mitume katika Yerusalemu walipojazwa na Roho Mtakatifu nao wakanena katika ndimi (Mdo. 2; M&M 109:36–37).