Misaada ya Kujifunza
Tamko Rasmi 1


Tamko Rasmi 1

Limepigwa chapa katika kurasa za kufungia za Mafundisho na Maagano, sehemu ya kwanza ya Tamko Rasmi 1 pia hujulikana kama Manifesto. Lilitolewa na Rais Wilford Woodruff na kuwasilishwa kwa waumini wa Kanisa katika mkutano mkuu mnamo 6 Oktoba 1890. Kuanzia mwaka 1862, sheria mbalimbali kwa miaka ishirini na mitano iliyofuatia ilifanya ndoa ya wake wengi ifanywe kuwa ni kinyume cha sheria katika Marekani. Bwana alimwonyesha Wilford Woodruff kwa ono na ufunuo nini kingetokea kama Watakatifu wasingeacha desturi ya ndoa ya wake wengi. Manifesto hiyo ilitangaza rasmi kwamba ndoa ya wake wengi haifanyiki tena.