Misaada ya Kujifunza
Funga, Kufunga


Funga, Kufunga

Kwa hiari kuacha kula au kunywa kwa madhumuni ya kujisogeza karibu na Bwana na kuomba baraka Zake. Wakati mtu binafsi na vikundi wafungapo, wanapaswa pia kusali ili kuyafahamu mapenzi ya Mungu na kukuza nguvu kubwa zaidi za kiroho. Kufunga daima kumekuwa kukifanywa na waumini wa kweli.

Katika Kanisa leo, siku moja ya Sabato kila mwezi imetengwa kwa madhumuni ya kufunga. Katika wakati huu, waumini wa Kanisa wanaacha kula chakula na kunywa maji kwa kipindi fulani. Kisha wao huchangia katika Kanisa fedha ambazo wao wangelizitumia kwa chakula kwa milo hiyo. Fedha hizi huitwa toleo la mfungo. Kanisa hutumia toleo hili la mfungo kwa kuwasaidia maskini na wenye shida.