Kufanya ibada zilizofanyika kwa mamlaka ya ukuhani duniani ziwe na nguvu mbinguni. Ibada zinatiwa mahuri zinapokuwa zimepokea idhini ya Roho Mtakatifu wa Ahadi, ambaye ni Roho Mtakatifu.
Kwao umetolewa uwezo wa kuwafunga kote mbinguni na duniani, M&M 1:8 .
Wale walio katika utukufu wa selestia wametiwa muhuri na Roho Mtakatifu wa Ahadi, M&M 76:50–70 .
Eliya anakabidhi funguo za uwezo wa kufunga katika mikono ya Joseph Smith, M&M 110:13–16 .
Huu ni uwezo wa kufunga na kuunganisha, M&M 128:14 .
Neno la unabii lililo imara zaidi linamaanisha kujua kwamba mtu ametiwa muhuri kwa uzima wa milele, M&M 131:5 .
Maagano yote yasiyotiwa muhuri na Roho Mtakatifu wa Ahadi yanakoma wakati wanadamu wanapokufa, M&M 132:7 .
Kazi kuu itakayofanyika katika mahekalu ni pamoja na kuunganishwa kwa watoto kwa wazazi wao, M&M 138:47–48 .