Msaada wa Masomo
Usimikaji
iliyopita inayofuata

Usimikaji

Kuchaguliwa na kuwekwa wakfu kwa madhumuni yaliyo matakatifu. Uteuzi huu ni kwa utumishi maalumu ndani ya muundo wa Kanisa kwa kuwekewa mikono na mtu aliye na mamlaka sahihi. Wale tu wanaosimamia akidi za ukuhani hupokea funguo kutoka kwa kiongozi wa juu wanaposimikwa. Watu wanaosimikwa katika nafasi tofauti na marais wa akidi za ukuhani wanaweza kupokea baraka za ukuhani, lakini hakuna funguo wanazopewa pamoja na baraka ile.