Misaada ya Kujifunza
Wamormoni


Wamormoni

Jina la utani la Mormoni liliundwa na watu ambao hawakuwa waumini wa Kanisa ili kuwataja waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Jina hili linatokana na kitabu kitakatifu cha maandiko yaliyokusanywa na nabii wa kale Mormoni na kuitwa Kitabu cha Mormoni. Jina lililotolewa na Bwana ambalo kwalo waumini wa Kanisa wanajulikana ni “Watakatifu.” Jina sahihi la Kanisa ni Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.