Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 60


Sehemu ya 60

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, katika Independence, Wilaya ya Jackson, Missouri, 8 Agosti 1831. Katika tukio hili wazee ambao walisafiri kwenda Wilaya ya Jackson na kushiriki katika uwekaji wakfu wa ardhi na kiwanja cha hekalu walitamani kujua kile walichotakiwa kufanya.

1–9, Wazee wahubiri injili katika mikutano ya waovu; 10–14, Wasiupoteze bure muda wao, wala wasivizike vipaji vyao; 15–17, Wanaweza kusafisha miguu yao kama ushuhuda dhidi ya wale wanaoikataa injili.

1 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwa wazee wa kanisa lake, ambao wanalazimika kurejea haraka kwenye nchi walikotoka: Tazama, imenipendeza Mimi, kwamba mje mahali hapa;

2 Lakini kwa wengine sipendezwi nao, kwani hawafungui avinywa vyao, bali bwanaficha vipaji ambavyo nimewapa, kwa sababu ya ckumwogopa mwanadamu. Ole wao hao, kwani hasira yangu inawaka dhidi yao.

3 Na itakuwa kwamba, kama wasipokuwa waaminifu zaidi juu yangu, akitachukuliwa, hata kile walicho nacho.

4 Kwani Mimi, Bwana, natawala katika mbingu juu, na miongoni mwa amajeshi ya duniani; na katika siku ile nitakapowafanya kuwa bhazina yangu, watu wote watajua ni nini kinachoonyesha uwezo wa Mungu.

5 Lakini, amini, nitasema nanyi juu ya safari yenu kwenda kwenye nchi mlizotoka. Na jengeni au nunueni mashua, kama muonavyo kuwa ni vyema, siyo muhimu kwangu, fungeni safari yenu upesi kwenda sehemu iitwayo St. Louis.

6 Na kutoka huko watumishi wangu, Sidney Rigdon, Joseph Smith, Mdogo, na Oliver Cowdery, washike safari yao kuelekea Cincinnati;

7 Na katika mahali hapo wapaze sauti zao na kulitangaza neno langu kwa sauti kubwa, bila ghadhabu wala mashaka, huku wakiinua mikono amitakatifu juu yao. Kwani ninaweza kuwatakasa, na bmmesamehewa dhambi zenu.

8 Na waliobaki wafanye safari yao kutokea St. Louis, wawili wawili, na wakihubiri neno, bila kuharakisha, miongoni mwa mikutano ya waovu, hadi warejee kwenye makanisa waliyotoka.

9 Na haya yote ni kwa manufaa ya makanisa; kwani ni kwa kusudi hili nimewatuma hao.

10 Na mtumishi wangu aEdward Partridge na atoe fedha ambazo nimempa, sehemu kwa wazee wangu ambao nimewaamuru kurudi;

11 Na yule ambaye ana uwezo, na arudishe kwa njia ya wakala; na yule asiye na uwezo, hahitajiki.

12 Na sasa ninasema juu ya waliosalia ambao watakuja katika nchi hii.

13 Tazama, wao wametumwa kuhubiri injili miongoni mwa mikutano ya waovu; kwa hiyo, ninawapa wao amri, kwamba: aUsipoteze muda wako bure, wala usizike btalanta yako ili isiweze kujulikana.

14 Na baada ya kuja katika nchi ya Sayuni, na kuwa umelitangaza neno langu, utarejea upesi, kulitangaza neno langu miongoni mwa mikutano ya waovu, siyo katika haraka, wala katika aghadhabu wala mabishano.

15 Na kungʼuta avumbi la miguu yako dhidi ya wale wasiokupokea, siyo mbele yao, usije ukawaudhi, bali sirini; na uoshe miguu yako, kama ushuhuda dhidi yao katika siku ya hukumu.

16 Tazama, hii inatosha, na ni mapenzi ya yule aliyewatuma.

17 Na kwa kinywa cha mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, itajulikana juu ya Sidney Rigdon na Oliver Cowdery. Yaliyosalia baada ya hii. Hivyo ndivyo. Amina.