Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 79


Sehemu ya 79

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, huko Hiram, Ohio, 12 Machi 1832.

1–4, Jared Carter anaitwa kuhubiri injili kwa msaada wa Mfariji.

1 Amini ninawaambia, kuwa haya ndiyo mapenzi yangu kwamba mtumishi wangu Jared Carter aende tena katika nchi za mashariki, kutoka mahali hadi mahali, na kutoka mji hadi mji, katika uwezo uliotokana na akutawazwa kwake, akitangaza habari njema za shangwe kuu, hata injili isiyo na mwisho.

2 Nami nitamletea aMfariji, atakaye mfundisha ukweli na kumwonyesha njia ya kwenda;

3 Na kadiri atakavyokuwa mwaminifu, nitamtuza tena miganda.

4 Kwa hiyo, moyo wako na ufurahi, mtumishi wangu Jared Carter, na ausiogope, asema Bwana wako, hata Yesu Kristo. Amina.