Sehemu ya 2
Dondoo kutoka katika historia ya Joseph Smith kuhusiana na maneno ya malaika Moroni kwa Joseph Smith Nabii, wakiwa ndani ya nyumba ya magogo ya akina Smith huko Palmyra, jioni ya Septemba 21, 1823. Moroni alikuwa wa mwisho katika safu ndefu ya wanahistoria ambao walitengeneza kumbukumbu ambayo sasa iko mbele ya ulimwengu kama Kitabu cha Mormoni. (Linganisha na Malaki 4:5–6; pia sehemu ya 27:9; 110:13–16; na 128:18.)
1, Eliya ataufunua ukuhani; 2–3, Ahadi za baba zapandikizwa katika mioyo ya watoto.
1 Tazama, nitaufunua kwenu Ukuhani, kwa mkono wa Eliya, nabii, kabla ya kuja kwa siku ile kuu na ya kutisha ya Bwana.
2 Naye atapandikiza katika mioyo ya watoto ahadi zilizofanywa kwa baba, na mioyo ya watoto itawageukia baba zao.
3 Kama si hivyo, dunia yote ingeliangamia kabisa wakati wa kuja kwake.