Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 35


Sehemu ya 35

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko au karibu na Fayette, New York, 7 Desemba 1830. Kwa wakati huu, Nabii alikuwa akijishughulisha karibu kila siku na kufanya tafsiri ya Biblia. Tafsiri hiyo ilianza mapema Juni 1830, na wote Oliver Cowdery na John Whitmer walikuwa wametumika kama waandishi. Kwa vile wote sasa walikuwa wameitwa kwenye majukumu mengine, Sidney Rigdon aliitwa kwa uteuzi ulio mtakatifu kuwa kama mwandishi wa Nabii katika kazi hii (ona aya ya 20). Kama utangulizi katika kumbukumbu yake ya ufunuo huu, Historia ya Joseph Smith inaeleza: “Mnamo Desemba Sidney Rigdon alikuja [kutoka Ohio] ili kumwomba Bwana, na pamoja naye alikuja pia Edward Partridge. … Muda mfupi baada ya kuwasili kwao ndugu hawa wawili, na hivi ndivyo alivyosema Bwana.”

1–2, Ni kwa namna gani watu wanaweza kufanyika wana wa Mungu; 3–7, Sidney Rigdon ameitwa kubatiza na kutoa Roho Mtakatifu; 8–12, Ishara na miujiza hufanyika kwa imani; 13–16, Watumishi wa Bwana watawapura mataifa kwa uwezo wa Roho; 17–19, Joseph Smith anashikilia funguo za siri; 20–21, Wateule watastahimili siku ya ujio wa Bwana; 22–27, Israeli ataokolewa.

1 Sikilizeni sauti ya aBwana Mungu wenu, hata bAlfa na Omega, mwanzo na mwisho, ambaye cuelekeo wake ni imara milele, yeye dyule leo kama jana, na hata milele.

2 Mimi ndimi Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, aaliyesulubiwa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, hata wale wote bwatakaoliamini jina langu, kwamba waweze kuwa cwana wa Mungu, hata dwamoja ndani yangu kama Mimi tulivyo ewamoja na Baba, vile Baba yu ndani yangu ili tuweze kuwa wamoja.

3 Tazama, amini, amini, ninasema mtumishi wangu Sidney, nimekuangalia wewe na kazi zako. Nimezisikia sala zako, na nimekutayarisha kwa kazi iliyo kuu.

4 Umebarikiwa wewe, kwani utafanya mambo makubwa. Tazama wewe umetumwa, kama vile aYohana, kuitengeneza njia mbele yangu, na mbele ya bEliya ambaye atakuja, na wewe hujui.

5 Na wewe umebatiza kwa maji kwa ajili ya toba, lakini ahawakumpokea Roho Mtakatifu;

6 Lakini sasa ninakupa wewe amri, kwamba autawabatiza kwa maji, na watampokea bRoho Mtakatifu kwa kuwekewa cmikono, kama vile mitume wa kale.

7 Na itakuwa kwamba kutakuwa na kazi kubwa katika nchi, hata miongoni mwa aWayunani, kwani upumbavu wao na machukizo yao yatakuwa dhahiri machoni pa watu wote.

8 Kwani Mimi ni Mungu, na mkono wangu ahaujafupishwa; na nitaonyesha bmiujiza, cishara, na maajabu, kwa wale wote dwaaminio katika jina langu.

9 Na yeyote atakayeomba kwa aimani katika jina langu, bwatawatoa cpepo wabaya, dwatawaponya wagonjwa; watawafanya vipofu kuona, na viziwi kusikia, na mabubu kusema, na viwete kutembea.

10 Na saa yaja haraka ambapo mambo makuu yataonyeshwa kwa wanadamu;

11 Lakini apasipo imani hakuna kitu chochote kitakachoonyeshwa isipokuwa bukiwa juu ya cBabilonia, ule ule ambao ulifanya mataifa yote kunywa mvinyo wa ghadhabu ya duasherati wake.

12 Na ahakuna yeyote afanyaye yaliyo mema isipokuwa wale walio tayari kupokea utimilifu wa injili yangu, ambayo nimeitoa kwa kizazi hiki.

13 Kwa hiyo, nimewachagua walio awadhaifu wa ulimwengu, wale ambao bhawakusoma na waliodharauliwa, ili kuyapura mataifa kwa uwezo wa Roho wangu;

14 Na mkono wao utakuwa mkono wangu, na nitakuwa angao yao na kigao chao; na nitafunga viuno vyao, watapigana kiume kwa ajili yangu; na bmaadui zao watakuwa chini ya miguu yao; na Mimi cnitaushusha upanga kwa niaba yao, na kwa dmoto wa hasira yangu nitawalinda.

15 Na amaskini na bwanyenyekevu watahubiriwa injili, nao cwatautazamia wakati wa ujio wangu, kwani u dkaribu

16 Nao watajifunza mfano wa amtini, kwani hata sasa wakati wa mavuno tayari u karibu.

17 Na nimepeleka autimilifu wa injili yangu kwa mkono wa mtumishi wangu bJoseph; na katika unyonge nimembariki;

18 Na nimempa afunguo za siri ya mambo byaliyofungwa, hata mambo yaliyokuwepo tangu cmisingi ya ulimwengu, na mambo yatakayokuja, tangu wakati huu hadi wakati wa ujio wangu, kama atakaa ndani yangu, na kama siyo, mwingine nitampanda mahali pake.

19 Kwa hiyo, utamwangalia yeye kwamba imani yake isitindike, na itatolewa na aMfariji, bRoho Mtakatifu, ajuaye mambo yote.

20 Na amri ninakupa wewe—kwamba autaandika kwa ajili yake; na maandiko yatatolewa, kama vile yalivyo moyoni mwangu, kwa wokovu wa bwateule wangu;

21 Kwani wataisikia asauti yangu, na kuniona Mimi, na wala hawatakuwa wamelala, nao bwatakaa siku ya cujio wangu; kwani watatakaswa, kama vile mimi dnilivyotakasika.

22 Na sasa aninakuambia, kaa pamoja naye, naye atasafiri pamoja na wewe; wala usimwache, na hakika mambo haya yatatimia.

23 Na kwa akuwa huandiki, tazama, itatolewa kwake yeye kutoa unabii; nawe utahubiri injili yangu na kuwataja bmanabii watakatifu ili kuthibitisha maneno yake, kama yatakavyotolewa naye.

24 aShika amri na maagano yote ambayo kwayo mmefungwa; na Mimi nitazifanya mbingu bzitikisike kwa ajili yenu, na cShetani atatetemeka, na Sayuni ditafurahi juu ya milima na kustawi;

25 Na aIsraeli bataokolewa katika wakati wangu mwenyewe utakapofika; na kwa cfunguo nilizompa wataongozwa, na wala hawatachanganyika tena kamwe.

26 Inueni mioyo yenu na furahini, aukombozi wenu u karibu.

27 Msiogope, enyi kundi dogo, aufalme ni wenu hadi nitakapokuja. Tazama, bnaja haraka. Hivyo ndivyo. Amina.