Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 126


Sehemu ya 126

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, katika nyumba ya Brigham Young, huko Nauvoo, Illinois, 9 Julai 1841. Kwa wakati huu Brigham Young alikuwa Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili.

1–3, Brigham Young anasifiwa kwa kazi zake na anapumzishwa kusafiri nje ya nchi katika siku zijazo.

1 Mpenzi na ndugu mpendwa, aBrigham Young, amini hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwako: Mtumishi wangu Brigham, haitakiwi tena mkononi mwako kuiacha familia yako kama siku zilizopita, kwa kuwa sadaka yako imekubaliwa kwangu.

2 Nimeona akazi na sulubu zako katika safari kwa ajili ya jina langu.

3 Kwa hiyo ninakuamuru kulipeleka neno langu nchi za nje, na utaishughulikia vizuri afamilia yako kutoka sasa, na kuendelea na milele. Amina.