Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 18


Sehemu ya 18

Ufunuo kwa Joseph Smith, Nabii, Oliver Cowdery, na David Whitmer, uliotolewa huko Fayette, New York, Juni 1829. Kulingana na Nabii, ufunuo huu uliojulikana kama “kuitwa kwa mitume kumi na wawili katika siku hizi za mwisho, na pia maelekezo yahusuyo kuanzishwa kwa Kanisa.”

1–5, Maandiko yanaonyesha namna ya kulijenga Kanisa; 6–8, Ulimwengu unakomaa katika dhambi; 9–16, Thamani ya nafsi ni kuu; 17–25, Ili kupata wokovu, wanadamu yawalazimu kujichukulia juu yao wenyewe jina la Kristo; 26–36, Wito na huduma ya Kumi na Wawili yafunuliwa; 37–39, Oliver Cowdery na David Whitmer wawatafute Kumi na Wawili; 40–47, Ili kupata wokovu, mwanadamu inamlazimu kutubu, kubatizwa na kushika amri.

1 Sasa, tazama, kwa sababu ya jambo ambalo wewe, mtumishi wangu Oliver Cowdery, umetaka kulijua kwangu, ninakupa maneno haya:

2 Tazama, nimekwisha jidhihirisha kwako, kwa Roho yangu mara nyingi, kwamba mambo ambayo umeyaandika ni ya akweli; kwa hiyo unajua ni ya kweli.

3 Na kama wewe unajua kwamba ni ya kweli, tazama, ninakupa wewe amri, kwamba utegemee mambo ambayo ayameandikwa;

4 Kwani katika hayo mambo yote yameandikwa kuhusu msingi wa kanisa langu, ainjili yangu, na bmwamba wangu.

5 Kwa hiyo, kama utalijenga kanisa langu, juu ya msingi wa injili yangu na mwamba wangu, milango ya jehanamu haitakushinda.

6 Tazama, aulimwengu unaiva katika dhambi; na ni lazima inahitajika kuwa wanadamu wachochewe katika toba, wote bWayunani na pia wa nyumba ya Israeli.

7 Kwa hiyo, kama aulivyobatizwa kwa mikono ya mtumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, kulingana na vile nilivyomwamuru, ametimiza jambo ambalo nilimwamuru.

8 Na sasa, usishangae kwamba nimemwita yeye kwa madhumuni yangu, madhumuni ambayo yanajulikana kwangu; kwa hiyo, kama atafanya abidii katika bkushika amri zangu catabarikiwa kwa uzima wa milele; na jina lake ni dJoseph.

9 Na sasa, Oliver Cowdery, ninasema na wewe, na pia na David Whitmer, kwa njia ya amri; kwani, tazama, ninawaamuru watu wote kila mahali kutubu, na ninasema nanyi, hata kama vile kwa Paulo amtume wangu, kwani mmeitwa kwa wito ule ule ambao yeye aliitwa.

10 Kumbuka athamani ya bnafsi ni kubwa mbele za Mungu;

11 Kwani, tazama, Bwana aMkombozi wako aliteseka hadi bkifo katika mwili; kwa hiyo caliteseka dmaumivu ya watu wote, ili kwamba watu wote waweze kutubu na kuja kwake.

12 Na yeye aamefufuka tena kutoka kwa wafu, ili kwamba aweze kuwaleta watu wote kwake, kwa masharti ya btoba.

13 Na ni ashangwe kubwa kiasi gani kwake katika nafsi ambayo hutubu!

14 Kwa hiyo, wewe umeitwa akutangaza toba kwa watu hawa.

15 Na kama itakuwa kwamba utafanya kazi siku zako zote katika kutangaza toba kwa watu hawa, na kuleta, japo iwe anafsi moja kwangu, shangwe yako itakuwa kubwa jinsi gani pamoja naye katika ufalme wa Baba yangu!

16 Na sasa, kama shangwe yako itakuwa kubwa kwa hiyo nafsi moja ambayo umeileta kwangu katika aufalme wa Baba yangu, itakuwa bshangwe kubwa namna gani kwako kama cutazileta nafsi nyingi kwangu!

17 Tazama, unayo injili yangu mbele yako, na mwamba wangu, na awokovu wangu.

18 aMwombe Baba katika bjina langu kwa imani, ukiamini kwamba utapokea, nawe utapata Roho Mtakatifu, ambaye hudhihirisha mambo yote yaliyo cmuhimu kwa wanadamu.

19 Na kama wewe hauna aimani, bmatumaini, na chisani, huwezi kufanya lolote.

20 aUsishindane na kanisa lolote, isipokuwa bkanisa la ibilisi.

21 Ujichukulie juu yako ajina la Kristo, na bsema ukweli katika cutulivu.

22 Na kadiri wengi wanavyotubu na akubatizwa katika jina langu, ambalo ni Yesu Kristo, na bkuvumilia hadi mwisho, hao ndiyo wataokolewa.

23 Tazama, Yesu Kristo ndilo ajina ambalo limetolewa na Baba, na hakuna jina lingine lililotolewa ambalo kwa hilo mwanadamu aweza kuokolewa;

24 Kwa hiyo, wanadamu wote yawalazimu kujichukulia juu yao jina ambalo limetolewa na Baba, kwani katika jina hilo wataitwa katika siku ya mwisho;

25 Kwa hiyo, kama wao hawajui ajina ambalo wanaitwa, hawawezi kupata nafasi katika bufalme wa Baba yangu.

26 Na sasa, tazama, wapo wengine ambao wameitwa kuihubiri injili yangu, kote kwa aMyunani na kwa Myahudi;

27 Ndiyo, hata kumi na wawili; na hao Kumi na Wawili watakuwa wanafunzi wangu, na wao watajichukulia juu yao jina langu; na hao aKumi na Wawili ni wale ambao hutamani kujichukulia juu yao bjina langu kwa dhamira ya moyo wao wote.

28 Na kama wao hutamani kujichukulia juu yao jina langu kwa dhamira ya moyo wao wote, hao wameitwa kwenda aulimwenguni kote kuhubiri binjili yangu kwa ckila kiumbe.

29 Na hao ndiyo wale ambao wametawazwa na Mimi akubatiza katika jina langu, kulingana na yale yaliyoandikwa;

30 Na wewe unayo yale ambayo yameandikwa mbele yako; kwa hiyo basi, ni lazima ufanye kulingana na maneno ambayo yameandikwa.

31 Na sasa ninasema na ninyi, aKumi na Wawili—Tazama, neema yangu inatosha kwenu; lazima mtembee wima mbele zangu na msitende dhambi.

32 Na, tazama, ninyi ndiyo wale ambao wametawazwa na mimi ili akuwatawaza makuhani na walimu; kuitangaza injili yangu, bkulingana na uwezo wa Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, na kulingana na cmiito na vipawa vya Mungu kwa wanadamu;

33 Na mimi, Yesu Kristo, Bwana wenu na Mungu wenu, nimeyasema haya.

34 aManeno haya si ya wanadamu wala mwanadamu, bali ni yangu; kwa sababu hiyo, mtayashuhudia hayo kuwa ni yangu na siyo ya mwanandamu;

35 Kwani ni asauti yangu ambayo huyasema kwenu; kwani yanatolewa kwa Roho yangu kwenu, na kwa uwezo wangu ninyi mnaweza kusomeana; na isingekuwa kwa uwezo wangu msingeweza kuyapata hayo;

36 Kwa hiyo basi, ninyi mnaweza akushuhudia kwamba mmesikia sauti yangu, na mnayajua maneno yangu.

37 Na sasa, tazama, ninatoa kwako wewe, Oliver Cowdery, na pia kwako David Whitmer, kwamba mtawatafuta Kumi na Wawili, ambao watakuwa na matamanio haya ambayo nimeyataja;

38 Na kwa matamanio yao na amatendo yao mtawajua.

39 Na mkiisha wapata mtaonyesha mambo haya kwao.

40 Na ninyi mtaanguka chini na akumwabudu Baba katika jina langu.

41 Na ninyi lazima mhubiri kwa ulimwengu, mkisema: Lazima mtubu na mbatizwe, katika jina la Yesu Kristo;

42 Kwani, watu wote lazima watubu na wabatizwe, sio tu wanaume, bali hata wanawake, na watoto ambao wamefikia umri wa awajibikaji.

43 Na sasa, baada ya kuwa ninyi mmepokea haya, ni lazima mzishike aamri zangu katika mambo yote;

44 Na kwa mikono yenu nitafanya akazi ya kushangaza miongoni mwa wanadamu, kwa bkuwashawishi wengi juu ya dhambi zao, ili waweze kuja kwenye toba, na ili waweze kuja kwenye ufalme wa Baba yangu.

45 Kwa hiyo basi, baraka ambazo ninazitoa kwenu ni ajuu ya mambo yote.

46 Na baada ya kupokea hii, kama ahamtashika amri zangu hamtaweza kuokolewa katika ufalme wa Baba yangu.

47 Tazama, Mimi, Yesu Kristo, Bwana wenu na Mungu wenu, na Mkombozi wenu, kwa uwezo wa Roho yangu nimeyasema haya. Amina.