Maandiko Matakatifu
Moroni 3


Mlango wa 3

Wazee wanawatawaza makuhani na walimu kwa kuwawekea mikono. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Njia ambayo wanafunzi, ambao waliitwa awazee wa kanisa, bwaliwatawaza makuhani na walimu—

2 Baada ya wao kuomba kwa Baba katika jina la Kristo, waliwawekea mikono, na kusema:

3 Katika jina la Yesu Kristo ninakutawaza uwe kuhani (au kama atakuwa mwalimu, ninakutawaza uwe mwalimu) kuhubiri toba na amsamaha wa dhambi kupitia kwa Yesu Kristo, kwa kuvumilia kwa imani kwa jina lake hadi mwisho. Amina.

4 Na katika njia hii awaliwatawaza makuhani na walimu, kulingana na bkarama na wito wa Mungu kwa watu; na waliwatawaza kwa cuwezo wa Roho Mtakatifu, ambaye alikuwa ndani yao.