Maandiko Matakatifu
Moroni 1


Kitabu cha Moroni

Mlango wa 1

Moroni anaandika kwa manufaa ya Walamani—Wanefi ambao hawatamkana Kristo wanauawa. Karibia mwaka 401–421 B.K.

1 Sasa mimi, aMoroni, baada ya kumaliza kufupisha historia ya watu wa Yaredi, sikudhania kama ningeandika zaidi, lakini bado sijafa; na sitaki kujionyesha kwa Walamani wasije wakaniangamiza.

2 Kwani tazama, avita vyao ni vikali sana miongoni mwao wenyewe; na kwa sababu ya chuki yao bwanaua kila Mnefi ambaye hatamkana Kristo.

3 Na mimi, Moroni, asitamkana Kristo; kwa hivyo, ninarandaranda popote niwezapo kwa usalama wa maisha yangu.

4 Kwa hivyo, ninaandika vitu vingine vichache, kinyume cha kile nilichotarajia; kwani nilidhani kuwa sitaandika zaidi ya hayo; lakini ninaandika vitu vichache zaidi, kwamba vingekuwa vya manufaa kwa ndugu zangu, Walamani, katika siku zijazo, kulingana na mapenzi ya Bwana.