Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 71


Sehemu ya 71

Ufunuo uliotolewa kwa Joseph Smith Nabii na Sidney Rigdon, huko Hiram, Ohio 1 Desemba 1831. Nabii alikuwa anaendelea kutafsiri Biblia akiwa na Sidney Rigdon kama mwandishi wake hadi ufunuo huu ulipopokelewa, wakati ambapo kazi hiyo iliwekwa kando kwa muda ili kuwawezesha kutekeleza maelekezo yaliyotolewa ndani yake. Viongozi hawa walitakiwa kwenda kuhubiri ili kutuliza hisia zisizo za kirafiki ambazo zilijitokeza dhidi ya Kanisa kama matokeo ya uchapishaji wa barua zilizoandikwa na Ezra Booth, ambaye alikuwa ameasi Kanisa.

1–4, Joseph Smith na Sidney Rigdon wanatumwa kwenda kutangaza injili; 5–11, Maadui wa Watakatifu watashindwa.

1 Tazama, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu watumishi wangu Joseph Smith, Mdogo, na aSidney Rigdon, kwamba amini wakati umekwishafika kwamba ni muhimu na yafaa kwangu kwamba ninyi mfungue vinywa vyenu katika bkutangaza injili yangu, mambo ya ufalme, na kuelezea csiri zake kutoka katika maandiko, kulingana na sehemu ya Roho na uwezo utakaotolewa kwenu, hata kama nitakavyotaka.

2 Amini ninawaambia, utangazieni ulimwengu katika maeneo ya jirani, na katika kanisa pia, kwa kipindi cha wakati, hata mpaka itakapojulishwa kwenu.

3 Amini kazi hii niwapayo ni ya muda.

4 Kwa hiyo, fanyeni kazi katika shamba langu la mizabibu. Waambieni wakazi wa dunia, na kuwashuhudia, na kutengeneza njia kwa amri na mafunuo ambayo yatakuja.

5 Sasa, tazama, hii ndiyo hekima; yeyote asomaye na aafahamu na bkupokea pia;

6 Kwani yule apokeaye atazidishiwa atele, hata uwezo.

7 Kwa hiyo, awashindeni maadui zenu; waiteni ili bwakutane na ninyi hadharani na faraghani; na kadiri mlivyo waaminifu aibu yao itajidhihirisha.

8 Kwa hiyo, na waje na hoja zao zenye nguvu dhidi ya Bwana.

9 Amini, hivyo ndivyo asemavyo Bwana kwenu—hakuna asilaha iliyotengenezwa dhidi yenu itakayofanikiwa;

10 Na kama mtu yeyote atapaza sauti dhidi yenu nitamshinda katika wakati wangu.

11 Kwa hiyo, zishikeni amri zangu; ni za kweli na za kuaminika. Hivyo ndivyo. Amina.