Maandiko Matakatifu
Mafundisho na Maagano 62


Sehemu ya 62

Ufunuo uliotolewa kupitia Joseph Smith Nabii, kwenye kingo za Mto Missouri huko Chariton, Missouri, 13 Agosti 1831. Siku hiyo, Nabii na kikundi chake, ambao walikuwa njiani wakitoka Independence kwenda Kirtland, walikutana na wazee kadha wa kadha waliokuwa njiani wakielekea zao katika nchi ya Sayuni, na, baada ya salamu za furaha, walipokea ufunuo huu.

1–3, Shuhuda zinaandikwa mbinguni; 4–9, Wazee wasafiri na kuhubiri kulingana na maamuzi yao na wanavyoelekezwa na Roho.

1 Tazama, na sikilizeni, Enyi wazee wa kanisa langu, asema Bwana Mungu wenu, hata Yesu Kristo, mtetezi wenu, ajuaye udhaifu wa mwanadamu na namna ya kuwasaidia wale wanaojaribiwa.

2 Na amini macho yangu yawaangalia wale ambao bado hawajaenda katika nchi ya Sayuni; kwa sababu hiyo huduma zenu bado hazijatimizwa.

3 Hata hivyo, mmebarikiwa ninyi, kwani shuhuda zenu mlizozitoa zimeandikwa mbinguni ili malaika wazione; nao hufurahi juu yenu, na dhambi zenu zimesamehewa.

4 Na sasa endeleeni na safari yenu. Jikusanyeni wenyewe juu ya nchi ya Sayuni; na pangeni mkutano na kufurahi pamoja, na kutoa sakramenti kwa Aliye Juu Sana.

5 Na halafu mnaweza kurudi na kutoa ushuhuda, ndiyo, hata nyote kwa pamoja, au wawili wawili, kama mtakavyoona kuwa ni vyema, si kitu kwangu; isipokuwa tu kuweni waaminifu, na tangazeni habari njema kwa wakazi wa dunia, au miongoni mwa makusanyiko ya waovu.

6 Tazama, Mimi, Bwana, nimewaleta ninyi pamoja ili ahadi ipate kutimilika, kwamba waaminifu miongoni mwenu yapaswa walindwe na kufurahi pamoja katika nchi ya Missouri. Mimi, Bwana, huwaahidi waaminifu na siwezi kuwadanganya.

7 Mimi, Bwana, niko radhi, kama mtu yeyote miongoni mwenu anataka kusafiri juu ya farasi, au juu ya nyumbu, au katika magari, atapokea baraka hizi, kama atapokea kutoka mkononi mwa Bwana, kwa moyo wa shukrani katika mambo yote.

8 Mambo haya yanabakia kwenu kufanya sawa sawa na maamuzi yenu na maelekezo ya Roho.

9 Tazama, ufalme ni wenu. Na tazama, na lo, mimi daima nipo pamoja na waaminifu. Hivyo ndivyo. Amina.